Je! Unatafuta Gauni Unayoweza Kuvaa Kokote Wakati Wowote? Jaribu Hii

Tuzungumze kuhusu nguo ambazo hazipitwi na wakati na zenye matumizi mengi, nguo ambazo zinashinda mitihani ya nyakati na mwenendo. Warembo, hauwezi kuonekana uko nje ya fasheni ukiwa umevaa gauni ambayo inakushepu vizuri umbo lako. Haijalishi kama unaenda ofisini, kwenye chakula cha jiioni ama sehemu za ibada.

Blossom Kitenge Dress by Tulivyo

Mara nyingi tunapenda kwenda na wakati na mitindo ya fasheni iliyopo kwa wakati huo, hakuna ubaya wowote juu ya hilo, ndio namna ulimwengu wa fasheni unavyofanya kazi na mitindo ni mengi na mipya kila mara lakini, tukiweza kuwekeza kwenye nguo ambazo hazitoki kwenye fasheni kama hiyo nguo pichani tutakua tumerahisisha maisha.

Kwa warembo wanaoenda kazini, unaweza kupata muonekano wa kiofisi kwa kuvaa hii nguo nzuri na koti jeusi, jekundi au jeupe ukavaa pia na viatu vyako vizuri vya visigino virefu vinavyoendana rangi na koti lako.


Blossom Kitenge Dress by Tulivyo

Hili gauni ni rahisi pia kulipangillia ukivaa kwenda kwenye hafla rasmi ya jioni na hata ile ya kawaida. Ipendezeshe zaidi kwa kuvaa cheni ya mkono ya dhahabu au ya fedha, sitoshauri kuvaa cheni ya shingoni na gauni hili kwasababu tayari shingo iko juu kidogo, lakini tusisahau herein zetu maridadi na viatu virefu, vyeusi, vyekundi ama vyeupe (binafsi ningeongeza umaridadi kwa kuivalia na viatu virefu vya kamba).

Tulivyo ipo kwaajili yako, njoo tukupe muonekano utakafanya uonekana kama unatoka kwenye maonesho ya mavazi.

Mlimbwende wetu amevaa nguo yetu kutoka Tulivyo inayopatikana kwa Shilling 60,000 tu. Bofya anuani hii kupata gauni hili:
www.tulivyo.co.tz/products/12